Wakati wa dirisha la usajili nchini Uingereza mambo mengi yalitokea, wengine waliumia sana lakini kuna wengine walifurahi mno. Hivyo ndivyo ilivyo pia kwa kocha Arsene Wenger dirisha lilimuumiza na kumfurahisha pia.
Wenger alifanikiwa kupambana hadi dirisha la usajili linaisha kumbakisha Alexis Sanchez ambaye ndio alikuwa kichwa cha habari katika usajili wa Arsenal wengi wakiamini alikuwa akiondoka Gunners.
Lakini hata hivyo Arsene Wenger aliwauza wachezaji wawili vijana Oxlade Chamberlain aliyekwenda Liverpool na mlinzi Kieran Gibbs ambaye amejiunga na klabu ya West Bromich Albion.
Wenger amekiri kwamba hawazi sana kuhusu usajili wa Oxlade Chamberlain lakini linapokuja suala la kumuwaza Kieran Gibbs huwa anaumia sana na kujiuliza ni kwa namna gani alimuachia aende West Brom.
“Ni kweli naumia kuhusu Gibbs kuliko Ox pia haswa ukizingatia kwa kuwa alifundishwa hapa tangu akiwa na miaka 10, hakuomba kuuzwa lakini katika umri wake hakika alihitaji sana nafasi za kucheza” alisema Wenger.
Wenger anaamini mchezaji kama Gibbs alikuwa zao muhimu sana kwao na alihitajika sana katika klabu hiyo lakini hakusita kumtakia kila la kheri katika klabu yake mpya ambako anaamini atapata nafasi.
No comments:
Post a Comment