MWANADADA anayefanya vizuri katika Bongo Fleva, Malaika Exavery ameeleza jinsi alivyotoswa huko Marekani, baada ya kuahidiwa kusimamiwa kazi zake, lakini asubuhi yake alipowafuata wahusika ili kuweka mambo sawa, wakamtosa.
Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Malaika alisema akiwa katika pub moja huko Los Angeles na marafiki zake wa Kitanzania, walimkutanisha na uongozi wa Justine Beiber kwa lengo la kusimamia kazi zake, wakakubali lakini kulipokucha jamaa hao walimweleza kwamba walimpa ahadi hiyo kwa sababu walikuwa mitungi na hawakuwa ‘siriaz’.
“Usiku jamaa walinihakikishia watasimamia kazi zangu, asubuhi na mapema nilikwenda kukutana nao ofisini kwao lakini waliniomba radhi kwa kile walichodai walinipa ahadi ile wakiwa ‘tungi’ hivyo natakiwa kusubiri hadi kumalizika kwa tour za Justine Beiber ili waangalie kama wanaweza kunisaini katika lebo hiyo,” alisema Malaika
No comments:
Post a Comment