Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amemkabidhi Obrey Chirwa majukumu ya Amissi Tambwe ambaye kwa sasa ni majeruhi.
Chirwa amepewa majukumu hayo kutokana na Tambwe kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya goti.
Kutokana na kuuguza majeraha hayo, ilisababisha Tambwe akose mechi tano za kimashindano ambazo tayari Yanga imecheza ikiwa moja ya Ngao ya Jamii na nne Ligi Kuu Bara.
“Kukosekana kwa Tambwe hakuna tatizo lolote lile kwani Chirwa yupo, ninachokifanya ni kwamba kwenye kikosi changu natengeneza ile hali kwamba akikosekana mmoja basi anakuwepo mwingine wa kuziba pengo lake,” alisema Lwandamina.
Obrey Chirwa
No comments:
Post a Comment