Msanii wa Bongo Flava kutoka kundi la Tip Top Connection, Dogo Janja hatimaye amefanikiwa kutimiza moja ya ndoto yake.
Dogo Janja anayehit na ngoma ya ‘Ngarenaro’ amefunguka hayo baada ya kukutana na mkali wa ‘Seduce Me’, Alikiba na kupiga naye picha.
“Alhamdulilah leo nimetimiza ndoto yangu ingine yakupiga picha na alikiba @officialalikiba #Ngarenaro Link In My Bio,” ameandika Jajaro baada ya kukutana na Alikiba jijini Arusha.
Alikiba na Dogo Janja ni moja ya wasanii watakoshambulia jukwaa la muziki la Fiesta linalotarajiwa kuanza rasmi katika Mkoa wa Arusha hapo kesho Jumamosi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
No comments:
Post a Comment