Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam zinaeleza mnamo tarehe 28.08.2017 majira ya saa kumi na moja jioni, lilimtia mbaroni mtuhumiwa HASHIMU RUNGWE SPUNDA kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Awali taarifa zilipokelewa toka kwa mlalamikaji aitwaye SULEIMAN YSIAN miaka 48, mfanyabiashara raia wa Uturuki kuwa alifika nchini akiongozana na kaka yake aitwaye ALI RIZA BELGEN wakitokea nchini Uturuki kwa madhumuni ya kufanya biashara ya kununua zao la korosho hapa nchini.
Walipokelewa na mwenyeji wao aliyemtaja kwa jina la SALUM MOHAMED waliyefahamiana akiwa nchini Uturuki, alimjulisha kuwa mmoja wa watu wanaojihusisha na biashara hiyo ya kuuza mazao ni ABDALA JUMA, hivyo alikwenda na kumtambulisha raia hao wa kituruki kwa ABDALA JUMA kama mfanyabiashara wa korosho. Na baada ya hapo ABDALA JUMA aliwachukua waturuki hao pamoja na mkalimani wao na kuwapeleka ofisini kwa mtu aliye mtambulisha kwao kwa jina la SALUM mmiliki wa kampuni ya LES TROPIQUES GROUP MINING SPRL LIMITED.
Raia hao wa kigeni walimweleza nia yao ya kununua korosho kiasi cha tani 15, na SALUM aliwahakikishia kuwa kampuni yake inauwezo wa kuwauzia korosho kwa kiasi kile walichohitaji.
Hivyo tarehe 09.11.2017 waliandaa mkataba baina ya ALI RIZA BILGEN na kampuni ya LES TROPIQUES GROUP MINING SPRL LIMITED. Hata hivyo muuzaji huyo wa korosho alimjulisha mteja wake kuwa anaomba kumshirikisha wakili wake katika makubaliano hayo. Tarehe 18.11.2017 walikwenda ofisini kwa wakili HASHIM RUNGWE SPUNDA ambaye alishuhudia makubaliano hayo na kuidhinisha.
Muuzaji huyo alimtaka mteja wake atume malipo ya awali ya kuandaa korosho hizo kupitia Acc.No.0250259097900 ya benki ya CRDB ambayo ni ya wakili HASHIM RUNGWE SPUNDA jambo ambalo mteja huyo alikubaliana nalo akiamini kuwa fedha hizo zitakuwa sehemu salama zaidi, mkataba unaonyesha gharama zote za manunuzi na usafirishaji ni jumla ya USD 72,000 ambazo zingelipwa kwa awamu tatu asilimia 20%, 20% na mwisho mzigo utakapofika Uturuki utamaliziwa 60%.
Mteja akiwa huko Uturuki tarehe 22.11.2016 alimtumia fedha HASHIMU RUNGWE kiasi cha USD 14,400 kwenye akaunti yake namba 0250259097900 ya CRDB, kama sehemu ya gharama za kushughulikia mzigo huo wa korosho. Baada ya kutuma fedha hizo ndugu ALI RIZA BILGEN, alimwomba wakili huyo akahakikishe kama kweli mzigo huo upo ama haupo, ndipo HASHIMU RUNGWE alipotaka alipwe kiasi cha USD 1,000 kama gharama za kwenda Lindi kuhakikisha uwepo wa korosho hizo na alipolipwa akasafiri na kisha kumjulisha mteja kuwa mzigo upo.
Baada ya uthibitisho huo kutoka kwa mtuhumiwa huyu, tarehe 12.12.2016 alitumiwa tena fedha kiasi kingine kiasi cha USD 15,400, katika akaunti yake ileile ya wakili huyo.
Aidha mteja huyo alipoona gharama zinazidi kuwa kubwa na hakuna mzigo unaoletwa kutoka Lindi, hivyo aliamua kurudi Uturuki. Walisubiri toka mwezi Novemba 2016 hadi April 2017 bila kupata chochote zaidi ya kuahidiwa tuu. Ndipo tarehe 20.04.2017 mteja alirudi tena nchini kujua kilichotokea safari hii ya pili hakumkuta mkalimani wao wa awali bali alipewa namba ya simu ya mkalimani mwingine aitwaye HUSSEIN SULEIMAN huyu alimpokea uwanja wa ndege na kumwezesha mawasiliano yote yaliyo kusudiwa.
Walikutana na muuzaji aliye dai kuwa kampuni yake iliingia matatani na serikali kuhusu masuala ya kodi hivyo hakuweza kusafirisha mzigo huo, badala yake alimwahidi kuwa angemuuzia ufuta badala ya korosho, pamoja na mabadiliko hayo muuzaji huyu alimtaka mteja wake warudi tena kwa wakili wake ili kuingia mkataba mpya.ndipo tarehe 25.05.2017 waliandaa mkataba mpya na kwenda ofisini kwa HASHIMU RUNGWE huko Kijitonyama kusaini mkataba huo wa ufuta ukishuhudiwa na wakili huyo.
Pamoja na mabadiliko hayo mnunuzi au mlalamikaji hakupata mzigo huo, badala yake muuzaji alikata mawasiliano na kutoweka.juhudi za kumkamata hazikufanikiwa hivyo aliamua kwenda kwa wakili huyo na kutaka kujua kilichomsibu mteja wake, ndipo wakili huyo alimtaka atoe kiasi cha USD 3,000 kama gharama za kufungua kesi mahakamani dhidi ya kampuni hiyo ya LES TROPIQUES GROUP MINING SPRL LIMITED.
Kwa kuwa mnunuzi tayari alikuwa amepoteza fedha nyingi mlalamikaji alimpatia kiasi hicho cha fedha wakili huyo, hata hivyo bado kesi haikufunguliwa, hivyo mnunuzi au mlalamikaji aligundua kuwa hata wakili anashiriki kumtapeli hivyo aliamua kufika Polisi ili kupata msaada katika jambo hilo.
Baada ya taarifa hizi kupokelewa kituoni uchunguzi ulianza mara moja ili kulinda heshima ya nchi kwa raia wa kigeni, polisi walifanikiwa kumkamata kwa mahojiano na kugundua kuwa amejipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Upelelezi unaendelea mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana ya Polis
No comments:
Post a Comment