Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu yamuachia huru Gwajima - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Friday 15 September 2017

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu yamuachia huru Gwajima




 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake katika kesi ya silaha baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka.
Ni takribani miaka miwili na nusu ambapo leo September 15, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake katika kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha na kuamuru Gwajima arudishiwe begi lake lenye risasi, bunduki na mali nyingine kwa sababu hakuna ushahidi kwamba alizembea kuhifadhi.
Mbali ya Gwajima, wengine waliochiwa huru ni mfanyabiashara anayedaiwa kuwa Mlinzi wake, George Mzava, Msaidizi wake, Yekonia Bihagaze na Mchungaji Georgey Milulu.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema>>>”Nimelazimika kuwaachia washtakiwa wote kwa sababu kesi dhidi yao haijathibitika katika viwango vilivyotakiwa.”
Alisema kuwa ni wazi kwamba mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Gwajima, aliripoti mwenyewe March 27, 2015 katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa ZCO ambapo alifanya hivyo akiwa na begi lake mkononi, ambapo hadi anafika kwa ZCO alikuwa hakukaguliwa na askari yeyote.
Pia katika ushahidi wa kesi hiyo iliyokuwa na mashahidi 10, Hakimu amesema hakuna askari aliyeeleza kama Gwajima alifanyiwa ukaguzi kabla ya kuonana na ZCO ambapo alisema Jamhuri haikupinga kama Gwajima alizimia na kwamba alikuwa makini na timamu kuhakikisha yupo na bunduki na begi lake hata alipolazwa hospitali.
>>>”Hivyo nawaachilia washtakiwa wote kwamba kesi dhidi yao mashtaka hayajathibitika. Pia naamuru begi, risasi na mali zote za Gwajima zirudishwe kwake kwa sababu hakuna uthibitisho wowote katika hilo.”
Katika kesi hiyo inadaiwa kati ya March 27 na 29, 2015 Dar es Salaam, Gwajima alishindwa kuhifadhi silaha aina ya Beretta namba CAT 5802 , risasi tatu za pistol na risasi 17 za Short Gun.
Shtaka la pili na la tatu linawakabili washtakiwa waliobaki ambao wanadaiwa kwamba March 29, 2015 katika Hospitali ya TMJ Mikocheni ‘A’ walikutwa wakimiliki silaha na risasi hizo bila ruhusa kutoka mamlaka husika.

No comments:

Post a Comment