
Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametoa
idhini ya wanawake kuendesha magari, hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza
katika historia ya taifa. Uamuzi huu umefikiwa kutokana na harakati za
muda mrefu kwa makundi ya wanawake na haki za bindamu kushinikiza
wanawake waruhusiwe kuendesha magari.
Kwa muda mrefu Saudi Arabia
imekuwa nchi pekee Duniani kuwazuia wanawake kuendesha magari. Abdallah
al-Mouallimi Mwakilishi wa umoja wa mataifa kutoka Saudia ametangaza
habari hizi umoja wa huko umoja mataifa."Ndugu Mwenyekiti, Mabibi na mabwana. Najua mtapenda kujua jambo hili kwamba dakika chache zilizopita Mfalme amepitisha sharia inayowapa idhini,wanawake nchini Saudia kuendesha magari.Hii ni historia mpya leo kwa jamii ya Saudia,kwa wanaume na wanawake.Na kwa sasa tunaweza kusema kitu angalau.'' Abdallah al-Mouallimi.
Mwanaharakati wa Saudi Arabia aliyewahi wekwa kizuizini kwa siku 73 kutokana na kupinga wanawake kuzuiwa kuendesha magari, ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter akisema 'Thank you God', yaani asante Mungu.
Sheria hii inaanza kufanya kazi mwezi june mwaka ujao, na kwa sasa wizara itatakiwa kuandaa ripoti maalumu kuhusiana na jambo hilo.
No comments:
Post a Comment