Mazungumzo kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na timu ya kutoka
Barrick Gold Corporation yameendelea leo Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yanafanyika kufuatia uchunguzi uliofanywa na tume mbili
zilizoundwa na Mhe. Rais Magufuli kuchunguza biashara ya madini ya
dhahabu na kubaini uwepo wa upotevu mkubwa fedha katika biashara ya
makinikia ya dhahabu ambayo husafirishwa kwenda nje ya nchi.
Wakati mazungumzo hayo yanaendelea wananchi wanataarifiwa kuwa na subira
na watajulishwa mara baada ya mazungumzo hayo kukamilika ama kwa hatua
yoyote itakayofikiwa.
Kamati Maalum ya Tanzania inayofanya majadiliano na timu kutoka Barrick
Gold Corporation inaongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba Prof.
Palamagamba Kabudi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment