Taharuki ikitanda baada ya tukio hilo.
WATU nane wamekufa na wawili wameokolewa wakiwa salama baada ya
Toyota Hiace kutumbukia Ziwa Victoria katika kivuko cha Kigongo Feri
wilayani Misungwi.“Kwa sasa uokoaji unaendelea, abiria wawili ndio wametoka salama. Maiti nane zimeopolewa,” amesema Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Mkoa wa Mwanza, Ferdinand Mshama.
Temesa ndiyo inasimamia kivuko hicho.
Mshama akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu amesema gari hilo linafanya safari kati ya Buhongwa jijini Mwanza na kivukoni hapo.
Amesema ajali hiyo imetokea kutokana na gari hilo kupata hitilafu kwenye mfumo wa breki hivyo liligonga geti la kivuko na kutumbukia ziwani.
Hiace iliyotumbukia ziwani.
Credit :goez to global publishers



No comments:
Post a Comment