Je McGregor "Notorious" Ataushangaza Ulimwengu Kwa Kumpiga Floyd Mayweather ? - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Friday 25 August 2017

Je McGregor "Notorious" Ataushangaza Ulimwengu Kwa Kumpiga Floyd Mayweather ?

Je McGregor "Notorious" Ataushangaza Ulimwengu Kwa Kumpiga Floyd Mayweather ?
Bondia mwenye uwezo wa hali ya juu ajulikanaye kama Conor MacGregor au Notorious kama anavyojulikana na mashabiki aliyemshawishi Floyd Mayweather "Unbeaten man" kutoka mafichoni alikokuwa na kuamua kurudi tena ulingoni ,je ataweza kuushangaza ulimwengu kwa kumkalisha Floyd ? au na yeye ataungana kwenye msululu wa wana masumbwi walioambulia kipigo kutoka kwa Floyd Mayweather ?


Hili ndilo swali ambalo lipo vichwani mwa wapenzi wengi wa boxing duniani ,ingawaje asilimia kubwa ya mashabiki wa boxing wamempa Floyd Mayweather asilimia kubwa ya kushinda pambano hilo lakini bado kuna kundi kubwa la watu wanaamini Conor McGregor ataushangaza ulimwengu kwa kumgalagaza Floyd Mayweather


Conor McGregor ambaye atatimiza miaka 29 14 July mwaka huu anaamini Floyd Mayweather ni bondia mzuri lakini hilo halimzuii yeye kumpa kichapo Floyd.

Conor McGregor anacheza staili ya Southpaw ,pia amechanganya boxing na Taekwando wakati Floyd anacheza staili ya orthodox .

Floyd Mayweather mwenye umri wa miaka 40 ambaye siku chache zilizopita alimzawadia mtoto wake wa kiume gari la kifahari kwenye sherehe yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 16 aliandika kwenye ukurasa wake wa Tweeter kuhusu mpambano huo ambapo baadhi ya mashabiki wameona kama ni matusi fulani hivi kwa Mc Gregor .

Sasa swali linabaki ,je McGregor ataweza kumkalisha Floyd na kuushangaza ulimwengu kama vile Tyson Furry alivyomfanyia Wladmir Klitshko??

No comments:

Post a Comment